Washirika wa Marekani wameelezea kusikitishwa na uamuzi wa serikali ya Washington kusaidia kuwasilisha mabomu ya Cluster nchini Ukraine.
Marekani ilithibitisha siku ya Ijumaa kwamba itatuma mabomu hayo yenye utata nchini Ukraine, huku Rais Joe Biden akisema ni HOFU YA MABOMU YA CLUSTER UKRAINE YASABABISHA BIDEN KUKUTANA NA SUNAK WAZIRI MKUU WA UINGEREZA NA MFALME CHARLES "uamuzi mgumu."
Katika kukabiliana na hili, Uingereza, Canada, New Zealand na Uhispania pia zimezungumza dhidi ya matumizi ya silaha hiyo.
Zaidi ya nchi 100 zimepiga marufuku utumiaji wa mabomu ya vishada kwa sababu ya hatari zinazowakabili raia.
Mabomu haya yanatoa mabomu madogo ambayo yanaweza kuua watu katika maeneo ya jirani.
Mabomu ambayo hayajalipuka pia yako katika hali ambayo yanaweza kulipuka baada ya kuachwa ardhini kwa miaka mingi bila kulipuka.
Rais Biden alisema kwamba ilimchukua muda mrefu kufanya uamuzi huu, na pia alisema kuwa ``Waukraine wanaishiwa na risasi.''
Uamuzi huu umekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu bila kusita, na Amnesty International imesema kuwa mabomu ya makundi yanatishia maisha ya raia hata muda mrefu baada ya kumalizika kwa vita.
Source: BbcSwahili
No comments: