WHAT’S HOT NOW

ads header

Business

Theme images by kelvinjay. Powered by Blogger.

Search This Blog

Blog Archive

Follow on FaceBook

Life & style

Sports

MAGAZETI YA LEO JUMATATU HAYA HAPA

 


ENDELEA KUSIKILIZA KIPITI RADIO ONLINE






MAGAZETI YA LEO JUMAPILI HAYA HAPA


ENDELEA KUSIKILIZA KIPITI RADIO ONLINE

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS HAYA HAPA



ENDELEA KUSIKILIZA KIPITI RADIO ONLINE KWA KUI-PLAY HAPO PEMBENI



 

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI


 



ENDELEA KUSIKILIZA KIPITI RADIO ONLINE

PATA MAGAZETI YA LEO JUMATATU

 





Endelea Kusikiliza Kipiti Radio Online 🎧📻

HISTORY YA KABILA LA WASAFWA/JAMII

 HISTORY KIDOGO _ JAMII / KABILA LA WASAFWA 


Wasafwa ni kabila toka jamii ya wabantu wanaozungumza lugha yenye uhusiano wa moja kwa moja na kibantu yaani lugha ya kisafwa. 

Kwanza tuangalie nini au chanzo cha neno Safwa. 

Neno safwa; 

Kihistoria wasafwa ni watu wanaopenda sana kuishi maeneo yenye mvua nyingi na ubaridi,  hi ni kutokana na wao kuwa ni wakulima wa mazao yanayohitaji mvua mfano viazi mviringo,  vitunguu swaumu,  mahindi na numbu.  Historia inasema kwamba kulitokea vita baina ya wasafwa na jamii zilizowazunguka wakigombea maeneo ya kilimo.  Katika vita hiyo kuliibuka mapigano makali mno ambapo ilionekana kuna watu wanapigwa lakini hawafi.  Kwa kisafwa mtu asiekufa huitwa au hicho kitendo huitwa ASIFWA yaani hafi. Kwa maana nyingine ili umuombee mtu mabaya na afe unatamka "asafwa" . Na moja kwa moja jamii hiyo ikaitwa safwa yaani kabila la wasafwa. 


Asili na chimbuko la wasafwa. 

Zipo nadharia nyingi zinazoelezea asili na chimbuko la wasafwa toka mbeya ambao ndio wenyeji haswa wa mbeya.  Ikumbukwe hawa ni wabantu,  hivyo basi ni jamii za kibantu toka afrika magharibi. Lakini nadharia na masimulizi haya yamegawanyika kama ifuatavyo, 

1. Wasafwa ni wa kutoka ugogo dodoma. 

Nadharia hii inasaidiwa na ukweli hasa kwenye salamu,  kuna wasafwa wakisalimiana utaskia "mwagona gogo " , ambapo humaanisha kuwa wao ni kutoka ugogo Dodoma.  Tatizo ni kwamba hawana uthibitisho wa kutokua wabantu hivyo nadharia hii huwa butu katika ukweli ijapokua wao huwamini hivyo. 


2. Wasafwa ni kutoka ukinga makete. 

Hapa napo kuna ushahidi,  ambao unaelezea kuwa wasafwa ni jamii toka ukinga,  nadharia hii inashibishwa na salamu pamoja na wasafwa waishio kata ya ilungu,  igoma na ulenje mbeya vijijini.  Katika suala la salamu baadhi husalimiana "mwagona kinga " , wakimaanisha kuwa hujambo mtu toka ukinga.  Pia wao huamini kuwa ni matokeo ya msafwa,  mkinga,  mnyakyusa na muwanji.  Lakini nadharia hii Pia inashadadiwa na ukweli kwamba katika kata hizo ni kweli wapo wakinga wengi mno ambao kwa sasa hujiita wasafwa na wanafuata mila na taratibu za kisafwa. Ni dhahiri kuwa wapo watu na koo kama kyando,  swallo,  longopa, chaula,  Enea na nyingine nyiiingi ambazo ni matokeo ya wazee wao kuhamia usafwani hasa tarafa ya tembela mbeya vijijini. 


3. Wasafwa ni kutoka unyakyusani. 

Nadharia hii ipo katika salamu,  ambapo wapo wasafwa wanaosalimiana "mwagona hondya " ,

Wakimaanisha hujambo toka unyakyusani,  . Ikumbukwe wasafwa huwaita wanyakyusa "wahondya " , nadharia hii inashibishwa na watu waishio tarafa ya Tembela mbeya vijijini hasa ilungu na igoma. Ushahidi wa nadharia hii unashibishwa zaidi na masimulizi ya wazee yahusuyo watu wa ajabu waliokua wanakula watu wenzao,  kwa kisafwa waliitwa "Ayinga " . Hawa ni viumbe waliokua wanapatikana maeneo ya pembezoni mwa safu za mlima livingstone,  ambao walisababisha jamii za watu wa kule hasa mwakaleli kukimbilia mbeya vijijini hasa maeneo ya ilungu na igoma.  Mmoja wa wahanga hao ni ukoo wa Mwanginde Mkoma ambao unawakuta mwakaleli na ilungu mbeya vijijini.


Katika makala yangu ijayo nitawaleteeni masimulizi kuhusu watu wa ajabu waliokua wanakula wenzao huko usafwani na kuzunguka safu za mlima livingstone ambao Pia ni matokeo ya baadhi ya wanyakyusa wa enzi hizo kukimbilia usafwani. 


4. Wasafwa ni wasangu 

Hapa Pia salamu ndio ushahidi na kigezo cha Kwanza.  Hawa husalimiana "mwagona sangu "  , wakimaanisha hujambo mtu wa usangu.  Hawa ni wengi uyole,  mswiswi,  igurusi,  inyala na itewe.  Wao huamini kuwa ni matokeo ya msafwa na msangu kwa baba. Ikumbukwe kuwa msangu alishirikiana na mbena kumshambulia muhehe ambapo baada ya kushindwa akamvamia msafwa. 


5. Wasafwa ni kutoka Botswana. 

Nadharia hii inashadadiwa na maelezo ya ufanano wa wasafwa na watu wa Botswana hasa katika ngoma za asili kama nyimbo na mtindo wa maisha.  Inasemekana kuwa wasafwa walitoka Botswana wakaingilia Moja kwa moja njia ya msumbiji hadi makete kisha mbeya.  Wengine hudai kuwa waliingilia dodoma . Ugumu wa nadharia hii upo katika ubantu maana kama ni ubantu asilimia kubwa ya jamii za kusini mwa jangwa la Sahara ni wabantu. 


6.wasafwa ni kutoka nchini kongo. 

Hapa ndipo penye maelezo mapana maana hawa ni wabantu na kwa kuthibitisha hilo Zipo shahidi toka koo mbalimbali kama Mwatumbo na Mwanshinga. Ifahamike kuwa wapo wanaoamini mwanshinga ni msafwa mkinga na Mwatumbo ni msafwa wa uwanji . Lakini historia inaonesha kuwa hawa ni wasafwa toka kongo hasa misitu ya kongo,  ukweli huo unashibishwa na maelezo kwamba ,

Asili ya mwanshinga  Ni historia ndeeeefu ambayo kwa ufahamu na masimulizi hapa Ni kurudi nyuma yaani kutrace back the background of Safwa tribe. Ambapo tunaambiwa wasafwa Ni kabila toka kundi la makabila yafahamikayo kma wabantu wanaopatikana hasa kusini mwa jangwa la Sahara wazungumzao lugha ya kibantu yenye ladha ya ubantu Na muingiliano Na makabila mengine ya kibantu.


Hivyo basi historia inasema WASAFWA Na mwanshinga  kwa ujumla asili hasa Ni Africa magharibi hadi  Sudan kusini, Na baadae wanahama kwa sababu mbalimbali, Ndipo wanasafiri hadi CONGO ya Leo hasa misitu ya Congo na pembezoni. 


Baada ya miaka mingi WASAFWA Na mwanshinga kwa ujumla wanahamia mbeya kwa misafara miwili , ambapo mmoja unaingilia sumbawanga -tunduma hadi mbeya mjini Na baadae mbeya vijijini ya  Leo. 


Msafara mwingine unaingilia zambia- malawi- msumbiji Na kuingilia makete yaani ukinga hadi mbeya vijijini Na mjini Na hasaaa ukoo wa mwanshinga. Hawa na wengine wengi ndio wale wanaosalimia "mwagona kinga" . Wasafwa hawa wengi wao ni koo za kichifu na kwa maana hiyo hata Leo chifu wa mbeya ni msafwa wa jamii hii. 

Lakini zipo nadharia zingine husema walitokea Botswana ijapokua haina mashiko Sana.


Baadhi ya shahidi kuwa walitoka Congo na huko Sudan kusini ni uwepo wa majina kama  vile majina yapatikanayo Congo  WAMBI, NGATELEE, MWINGA, MBWIGA, SELINA , SILYELELO n.k.

PIA

Kitendo Na tabia ya kupenda kuishi maeneo yenye mvua nyingi kma vile mbeya , Arusha Na Kilimanjaro Ni sawa Na mvua zipatikanazo misitu ya kongo.

PIA kupenda kilimo haswa viazi mviringo. 

Misafara hiyo inasemekana ilitengana baada ya kutokea sintofahamu wakiwa njiani toka kongo,  walipofika njiani wengine wakasonga kuelekea Zambia,  malawi, msumbiji pembezoni mwa ziwa nyasa hadi makete ya Leo.  Huko wakakaa na kuishi wakichangamana na wenyeji yaani wakinga na wawanji na baadae watoto wanazaliwa na wengine kuhamia mbeya vijijini.  Hawa walikua ni wale wanaopenda kuhamahama na kwa kuwa tayari mbeya kulikua na wa safwa walioingilia Tunduma hadi mbeya mjini ikawa rahisi kwao kuingia mbeya kwa kupitia njia ya makete isyonje yaani hasa kata ya ilungu ambayo ilikua kama lango. 

pia  historia inaendelea kudai kuwa kundi la Wasafwa waliopitia Sumbawanga walikutana na wafipa wa Sumbawanga na wakaendelea na msafara kuelekea mashariki na baadaye ndio wanakuja wanakutana kwenye mgongano na wasangu ambapo muda huo kulikua na mvutano kati ya wasangu na wahehe chini ya mkwawa na hivyo wakaanza kusambaa maeneo ya  Mbeya.


Hitimisho. 

Wasafwa ni wabantu toka kusini mwa jangwa la sahara. Wasafwa toka mbeya ni mchanganyiko wa makabila kadhaa kutokana na muingiliano wa shughuli za kibinadamu. Lakini msafwa hasa ni yule mwenye asili ya kongo.  Ukweli ni kwamba vita,  njaa na ustaarabu vilipelekea wasafwa kuingiliana na jamii nyingine.  Mfano baada ya vita kati ya merere na chifu lyoto wa usafwa mabinti wawili wa kisafwa walitolewa kama zawadi kwa chifu merere baada ya kushinda.  Kwa hiyo msafwa asili asie na mchanganyiko enzi hizo ni yule wa mbeya mjini. 


MGAWANYIKO WA MAKUNDI YAUNDAYO KABILA LA SAFWA 

Wasafwa wamegawanyika katika makundi makubwa matano na kimaongezi au matamshi wamegawanyika katika makundi kumi.  Katika makundi hayo matano kuna ,

1. Wamporoto 

Hawa ni wasafwa wanaozungumza kisafwa chenye ladha tofauti na makundi mengine.  Hawa hupatikana kwa wingi na kwa kiasi mwakaleli number one,  kiwira,  isyonje,  ndaaga,  ntokela wilaya ya rungwe na baadhi ya maeneo ya maendeleo,  tembela na ijombe mbeya vijijini. 

Wao ni matokeo ya msafwa kwa wingi na mchanganyiko wa baadhi ya makabila. 


2. Wasongwe 

Ni wasafwa wazungumzao kisafwa chenye ladha ya kipekee na makundi mengine.  Hawa huzungumza na kuelewana zaidi wao kwa wao maana ni wasafwa wa songwe. Wanapatikana na kuishi kwa wingi mbalizi,  utengule usongwe,  mshewe,  usongwe,  swaya,  igale,  iwindi na maeneo ya wilaya ya mbozi. Pia wapo Tunduma na mbeya mjini kwa kuhamia. 

Pia 

Mmalila na Mnyiha kihistoria wote walitokana na koo za Wasafwa ambao walitawanyika kwa lengo kujihami/kuzuia kushambuliwa na Maadui wakati wa mapigano yaliyokuwepo enzi hizo. Wasafwa wa utengule na mshewe ndio hasa inaaminika ni matokeo ya mnyiha wa leo na mmalila. Kuna mzee alisema Wamalila wametokana na neno "Malila" yaani sehemu ambayo maadui walikuwa wanayoishia na lengo kuu ni kwenda kuzuia maadui sehemu wanazoishia na kwa upande wa "Wanyiha" anasema ni neno lililotokana na sehemu ambako maadui walielekea au kukimbilia wakati wa mapigano hivyo basi hata matamshi yalikuwa yanabadilika kwa kadiri walivyokuwa wanakutana na kuchangamana na jamii zingne huko walikoelekea.


3. Wagulukha 

Hawa wanaishi na kupatikana kwa wingi chunya,  ikukwa,  ihango,  lwanjiro na mbeya mjini.  Wao ni tofauti kidogo kimatamshi na wale wa maeneo mengine. Hawa wengi wameoa na kuolewa na wabungu toka chunya na kiasili wao ni matokeo ya vita kati ya merere na chifu lyoto mbeya mjini ya Leo. 


4.wambwila 

Hawa wanaishi na kupatikana kwa wingi ilungu,  igoma,  ulenje,  makete na mbeya mjini.  Hawa huzungumza kisafwa cha kipekee mno,  wao Pia ndio lango kuu la mkinga kuingia mbeya mjini. Wanazungumza zaidi kisafwa kiitwacho kimbwila. Wengi wao huishi nje ya mji yaani milimani kwenye mvua nyingi kwa ajili ya kilimo hasa mbeya vijijini.  Na kundi la mwisho ni 


5. Wamalila 

Upo utata kuhusu kundi hili kama ni kabila au kundi ndani ya kabila.  Ifahamike kuwa neno wamalila kwa kisafwa lina maana ya uchafu mwilini uliowekwa kishirikina yaani " amalila " .

Sasa ukiwauliza wamalila wao husema asili yao ni botswana na wengine husema ni mlima mbeya sababu ambayo ni sababu ya asili ya msafwa kufikia yaani mlima mbeya.  Kuhusu botswana historian haifafanui vyema. 

Ila 

Hili ni kundi ambalo kwa wasafwa ni kundi lililojitenga na wenzao kwa kiasi.  Wanaishi tarafa ya isangati yote na maeneo ya usongwe. 


pia katika kundi la wamalila kuna wamalila wapo kule na ushahidi  wa kuthibitisha waliendaje kule ni kwamba ,

katika kipind cha mgogoro na mtemi merere kuna moja kati ya watu wa kisafwa alipambana kumuua askari mmoja wa mtemi merere na kukimbilia maeneo ya mbozi eneo hilo likiitwa ntandala na baadaye alioa huko ila hakuendelea kukaa huko aliamua kurudi ijapo hakufika eneo lake la nyumban ila huyo shujaa aliweza kuishi maeneo ya umalila na maisha yake yaliendelea hapoo alikuwa ni mtu kutoka ukooo wa Nswila watu wanopatkana kwa wingi maeneo ya iwindi hadi leo na kidogo umalila


Hitimisho 

Makundi haya yamegawanyika Pia katika matamshi,  mfano ndani ya kata moja unakuta kuna utofauti mdogo kimatamshi. 


NGOMA ZA ASILI 

ngoma kuu ya asili ya wasafwa ni ngoma ichezwayo wakati wa sherehe,  matambiko na mavuno.  Ngoma hii maarufu huitwa " mbeeta " . Huchezwa kwa kutumia filimbi,  pembe za wanyama,  mbegu zilizo ndani ya makopo na vingine vingi.  Ngoma za asili huchezwa kwa sasa hasa itewe, ikukwa na ifumbo.  Hakika kwa kule bado wanaenzi asili.


KILIMO 

Wasafwa ni kabila la wakulima ambao hulima sana viazi,  mahindi,  ngano,  numbu,  karanga,  maharage na mazao mengine kama miti.  Wasafwa Pia ni wafanyabiashara hasa viazi na vitunguu swaumu. Wasafwa hulima sana maeneo yenye mvua nyingi kama rungwe na mbeya vijijini. 

Pia hujishughulisha na biashara 


Kutokana na kilimo wametawanyika Tanzania na kwenda maeneo yenye mvua,  wapo kwa wingi Arusha hasa Arusha chini na meru,  wapo mang'ola karatu,  muheza Tanga,  west kilimanjaro,  usa Arusha,  muffindi iringa,  njombe,  makete na morogoro. 


WASAFWA NA MBEYA 

Neno mbeya ni neno litokanalo na lugha ya kisafwa likiwa linatamkwa ibheya likimaanisha chumvi.  Wafanyabiashara walifika mbeya na kubadilishana chumvi toka chunya na mlima mbeya kwa bidhaa nyingine.  Ilikua ni ngumu wageni kutamka neo ibheya na hivyo wakajikuta wanatamka imbeya.  Baadae miaka ya 1927 wakati wa usanifishaji wa kiswahili neno hilo likasanifishwa na kuwa mbeya. 

Pia 

Maneno asilimia 90 ya maeneo ndani ya jiji la mbeya yanatafsiriwa kwa kisafwa. 

Mfano neno mbalizi _ mbalisi 

Loleza _ lolezya (sindikiza)

Uyole _ iyoole 

Igawilo _ kigavilo ( sehemu ya kugawania )

Isyesye _ inzyesye 

Iwambi _ wambi 

Ijombe _ aina ya mti 

N. k 

Kiongozi mkuu wa kimila huitwa Mwene na kwa sasa Mwene ni Rockety mwanshinga.  


MAJINA YA WASAFWA 

Majina ni sehemu ya utamaduni wa wasafwa,  mtoto hupewa jina kutokana na tukio au kumbukumbu flani.  Mfano mtu akiitwa Nzala,  huyo alizaliwa kipindi cha njaa. 

Mbwiga _ mtoto wa kiume aliekua kwa kuumwa umwa na kupewa madawa 

Mbozyo _ mtoto wa kike aliekua kwa kuumwa umwa na kutibiwa kwa miti shamba 


Pia kuna jina kwa Kisafwa "Nkundi'. 

Jina hili anapewa mtoto ambaye watangulizi wake wote wamefariki.  Zamani kulikuwa na shida kubwa ya kufa watoto kwa mfuatano katika familia,  na kwahiyo basi mtoto aliyekua vyema alipewa jina la Nkundi, maana ya Inkundi kisafwa ni vumbi.  Sasa wazazi walitoa jina hilo kwa kuonesha kukata tamaa kuwa hata huyo aliyezaliwa atakuwa mali ya vumbi.


"Esose' kwa Kisafwa maana yake ni kuzaa mtoto asiye na baba rasmi. Zamani hii ilikuwa ni tukio la nadra sana  na ilionekana ajabu sana  kusikia binti wa fulani "asosile umwana"

Vinginevyo siku za huku baadaye majina haya yamekuwa yakitumiwa tofauti na maana zake halisi kutokana na ukweli kwamba akina bibi wanarithisha majina yao ili yaendelee kuwepo hata baada ya wao kutoweka. 


Wapo watoto sasa hivi wanaitwa 'Matundu' bila maana halisi ya neno hilo. 

Matundu kwa kisafwa ni majani ya mmea wowote. Mtu alipoitwa Matundu ilimaanisha kuwa amepatikana kwa njia za madawa ya majani asilia. 


Pia yapo majina ya koo na mengi huwa na MWA...... mwanzoni mfano mwalingo,  mwanyanje,  mwaihoyo,  mwantinda,  mwandele,  mwanzanga,  mwasote,  mwanzanga,  mwangoka,  mwanandodo,  mwaanzala , mwanyonga , mwanzonga , mwalyambi ,mwajafu,  mwansanga , mwanguku , mwaamudu, mwalyego, mwandiya , mwasoni, n. k. 

Pia wapo akina 

manzozi,  magwilla,  sijanga,  sijonjo,  simwinga,  yilyelelo,  ndabhishe,  masimbani , lyoto , lingo, Ngatele , Ndaduu, Ndilwene , Ndangano, Gwilla , zyoni ,malema , nzalu,  sewa,  selina, Nsolo,  sambwe , nzambwe , mponzi , zella , Ndongole ,Nzongwa, shitambala,   fwokile,  selela,  na mengine meeengi. 


Siku hizi watoto wengi wa mbeya yaani wakisafwa hupewa majina kutokana na ama baba ni mpenzi wa mchezaji fulani au mwanamziki.  Wapo kwa sasa watoto huitwa Ronaldo,  Beckham,  Rooney,  Nelly,  Awilo, Yesu,  lowasa,  kikwete,  mess,  Zidane na mengine meengi 


DINI NA MIUNGU 

Wasafwa wengi wao ni wakristo na wapagani.  Ni ngumu sana kumkuta msafwa mwislamu. Wale wapagani husali maeneo ya misitu maarufu "maganjo " kama lile lililopo pale jijini mbeya.  Wengi bado wanaamini katika miungu.  Ni ukweli kwamba 50% ya wasafwa ni wakristo na 50% wapagani.  


Uchawi mkuu kwa wasafwa huitwa ITUNGA  na wale wauaji wa kichawi huitwa MBUDA.  Mambo haya ni ya kimila hivyo imekua ngumu sana kuwabadilisha baadhi ya watu .


Yapo mengi sana kuhusu wasafwa na mbeya yao,  ila kwa kuhitimisha tu kwa hii historia fupi ni kwamba hawa wasafwa ndio wenyeji wa mbeya.  Ni wabantu wazungumzao kisafwa kibantu. 

Salamu yao kuu ni Mwagona.


Shukrani za pekee kwa wazee wote niliopata simulizi zao wakiongozwa na babu zangu,  bibi na watalamu kadhaa.  Pia heshima kwa wote mlioongezea kwenye groups mbalimbali.  Kama una nyongeza karibu sana


CREDIT: MBUZA MBASHA ALLEN


PATA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI



 



HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 15,2023





"NCHI HAIUZWI WALA BANDARI WAPUUZWE WENYE NIA MBAYA" DKT TULIA



"NCHI HAIUZWI WALA BANDARI WAPUUZWE WENYE NIA MBAYA" DKT TULIA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi kupuuza hoja za baadhi ya watu wenye nia ovu wanaosema kwamba Serikali inampango wa kuuza Bandari ya Dar es Salaam huku wakijua fika kuwa ni mashirikiano ya kibiashara yanayofanywa na si vinginevyo.


Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 14, Julai 2023 wakati wa mkutano wa hadhara alioufanya katika Kata ya Iyunga Jijini humo kwa lengo la kuwaelezea Wananchi baadhi ya ahadi alizozitekeleza katika Jimbo hilo ikiwemo Kata hiyo pamoja na yale yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita.


Amewaeleza kuwa katika kipindi chake cha Uongozi wa miaka miwili ndani ya Jimbo hilo kwa kushirikiana na Serikali wameweza kufanikisha utatuzi wa changamoto mbalimbali ikiwemo kuwezesha ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Inyala hadi Airport ambao utekelezaji wake umeshaanza.


Kuhusu changamoto ya maji na afya, Dkt. Tulia amewaeleza Wananchi hao kwamba Serikali imewezesha kupatikana kwa ufumbuzi huo kupitia mradi wa mto Kiwila ambao utamaliza tatizo hilo kwa Mkoa mzima wa Mbeya na kuhusu afya tayari Serikali imewezesha upatikanaji wa vifaa tiba katika Hospitali zote ndani ya Jiji hilo.


“Niwaombe sana, watu hawa wapuuzwe na niwahakikishie tupo salama na hakuna cha bandari wala nchi inayouzwa na hata wakija hao wanaosema imeuzwa waambieni wawapatie mgao wa hayo mauzo” Amesisitiza Dkt. Tulia.

HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO IJUMAA 14,2023

 





MAGAZETI YA LEO JUMANNE 11,2023

 





HOFU YA MABOMU YA CLUSTER UKRAINE YASABABISHA BIDEN KUKUTANA NA SUNAK WAZIRI MKUU WA UINGEREZA NA MFALME CHARLES


 Washirika wa Marekani wameelezea kusikitishwa na uamuzi wa serikali ya Washington kusaidia kuwasilisha mabomu ya Cluster nchini Ukraine.

Marekani ilithibitisha siku ya Ijumaa kwamba itatuma mabomu hayo yenye utata nchini Ukraine, huku Rais Joe Biden akisema ni HOFU YA MABOMU YA CLUSTER UKRAINE YASABABISHA BIDEN KUKUTANA NA SUNAK WAZIRI MKUU WA UINGEREZA  NA MFALME CHARLES "uamuzi mgumu."

Katika kukabiliana na hili, Uingereza, Canada, New Zealand na Uhispania pia zimezungumza dhidi ya matumizi ya silaha hiyo.

Zaidi ya nchi 100 zimepiga marufuku utumiaji wa mabomu ya vishada kwa sababu ya hatari zinazowakabili raia.

Mabomu haya yanatoa mabomu madogo ambayo yanaweza kuua watu katika maeneo ya jirani.

Mabomu ambayo hayajalipuka pia yako katika hali ambayo yanaweza kulipuka baada ya kuachwa ardhini kwa miaka mingi bila kulipuka.

Rais Biden alisema kwamba ilimchukua muda mrefu kufanya uamuzi huu, na pia alisema kuwa ``Waukraine wanaishiwa na risasi.''

Uamuzi huu umekosolewa na mashirika ya kutetea haki za binadamu bila kusita, na Amnesty International imesema kuwa mabomu ya makundi yanatishia maisha ya raia hata muda mrefu baada ya kumalizika kwa vita.

Source: BbcSwahili


VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI LEO JUMATATU 10,2023


 



MKURUGENZI WA KAMPUNI YA PLANCON LTD AKAMATWE

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Mohamed Hassan Moyo amemuagiza OCD wa wilaya ya Nachingwea kumkamata mara Moja mkurugenzi wa Kampuni ya Plancon Ltd Kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa bwawa la maji ya kunyweshea mifugo katika Kijiji cha Matekwe


Moyo amesema kuwa kampuni hiyo imeshindwa kukamilisha mradi wenye thamani ya Shilingi 405,757,160.00 ambao ulitakiwa kukamilika April 2022 lakini hadi sasa mradi huo haujakamilika


Alisema kuwa Bwawa hilo linauwezo wa kuhifadhi maji mita za ujazo 102,000 kwa wakati mmoja kulingana na hali ya mvua huku ikitarajiwa bwawa hilo litahudumia ng’ombe 9,992,mbuzi 2,711 na kondoo 489.


Mhe. Moyo amesisitiza kuwa mkurugenzi huyo popote pale alipo akamatwe apelekwe Nachingwea kukamilisha mradi wa Bwawa katika Kijiji cha Matekwe.


Akisisitiza hoja hiyo amesema haiwezekani Mhe. Rais analeta fedha Nachingwea alafu zitumike visivyo.

RC CHALAMILA KUTAKA ELIMU YA BIMA ITOLEWE KWA JAMII



RC CHALAMILA KUTAKA ELIMU YA BIMA ITOLEWE KWA JAMII


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo Julai 8, 2023 wakati akiongoza matembezi maalum kuanzia Mlimani City- Mwenge ITV na kuhitimisha tena viwanja vya Mlimani City, maarufu kwa jina la "Bima Walk" yenye lengo la kukuza uelewa kwa jamii kuhusu Bima, ambayo yameandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)


RC Chalamila ametaka hamasa zaidi na elimu kuhusu Bima itolewe kwa jamii ili wananchi wafahamu umuhimu na faida ya Bima lakini pia mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania kuja na ubunifu wa kuwa na vifurushi ambavyo vitakuwa rafiki kwa watu wa kipato cha chini.


Pia Mhe Chalamila ameelekeza matembezi mengine ya aina hiyo yafanyike katika maeneo yenye watu wengi kama Karikaoo, na Mbagala, vilevile amesistiza Viongozi wenye mamlaka mbalimbali kuwa mstari wa mbele kukata Bima kwa kuwa Bima ziko za aina mbalimbali mfano Bima ya Afya, Elimu, na Usalama wa biashara.


Kwa Upande wa Kamishna wa TIRA Dkt Baghayo Saqware amesema Mamlaka imeaandaa matembezi hayo ambayo yanafaida kiafya kwa kuwa mazoezi ni Afya lakini lengo kubwa ni kuelimisha na kuhamasisha jamii umuhimu na maana ya Bima kwa kuwa Bima inakinga dhidi ya majanga.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 9,2023